Nyota wa muziki kutoka Nigeria David Adedeji Adeleke maarufu kama Davido ameshinda tuzo ya msanii bora kutoka Afrika ‘Best African Act’ katika tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) zilizofanyika usiku wa jana katika uwanja wa Wembley kwenye ukumbi wa The SSE Arena jijini London Uingereza.

Davido amewapiku Wizkid, Babes Wodumo, C4 Pedro, Nyashinski na Nasty C ambao ni wasanii wa Afrika waliokuwa kwenye kipengele cha msanii bora wa Afrika kuwania tuzo hiyo.

Davido ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya unaoitwa ‘FIA’ aliweka ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter akiwashukuru mashabiki wake na mama yake.

 

Tyrese awaangukia mashabiki, ajuta kumwaga chozi hadharani
Trump achukia kuitwa 'mzee' na Kim Jong-un