Skelewu hitmaker, Davido kutoka Nigeria na mkali wa Ngololo, Diamond Platinumz watadhihirisha uswahiba wao kwa kuperform pamoja collabo yao ‘Number One Remix’ kwenye tuzo za MTV/MAMA2015 zitakazotolewa July 18, 2015, Durban, Afrika Kusini.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Davido amepost picha inayomuonesha yeye na Diamond wakiperform kwenye MTV/MAMA2014 na kuandika ujumbe unaoonesha kuwa mwaka huu pia watapiga show pamoja.
“PERFORMING AGAIN LIKE THIS AT ‪#‎MTVMAMA2015‬ !! TOO MUCH BLESSINGS…” Davido ameandika facebook.

MTV wametangaza majina ya wasanii waatakaongezeka kwenye jukwaa kupiga show kubwa itakayomshirikisha pia mkali wa RnB kutoka Marekani, Ne-Yo. Wasanii walioongezwa hivi karibuni ni Bucie, Cassper Nyovest, Diamond Platnumz, Davido na Yemi Alade.

Hii ni habari njema kwa mashabiki wa wasanii hao ambao waliwahi kuingia katika zogo la kutoelewana baada ya kudaiwa kuwa wasanii hao wana ‘beef’. Baadhi ya jumbe zilizokuwa zinawekwa kwenye mitandao ya kijamii na wasanii hao zilitafsiriwa kama njia ya kumchana adui.

Davido na Diamond wanawania tuzo hizo mwaka huu huku wakipigana vikumbo katika vipengele vya msanii bora wa kiume kinachowajumilisha pia Wizkid (Nigeria), AKA (Afrika Kusini) na Sarkodie (Ghana) na kipengele cha Best Collaboration.

Diamond anawania tuzo hizo katika vipengele vitatu ambavyo ni ‘Best Male’, Best Collaboration na Best Live.
Mtanzania unapaswa kumpigia Diamond na Vanessa Mdee anaewania kipengele cha Best Female. Piga kura zaidi ya mara 20 kwa siku. Unaweza kupiga kura kupitia link hii http://mama.mtv.com/voting/

'Nusu Nusu' ya Joh Makini yashika Namba 1 Chart ya MTV Base
Mkapa Awatahadharisha Wanaowania Uongozi