Mashirika ya kutoa msaada yamesema kuwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi zenye ladha tamu ya matunda ya ‘strawberry’ kwa ajili ya watoto zitaanza kutolewa katika nchi za Afrika kuanzia mwakani.

Dawa hizo zitakuwa ni dawa za kwanza zenye ladha tamu kukabiliana na na virusi vya ukimwi kupatikana kwa ajili ya watoto.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watoto milioni 1.5 kote duniani wanaishi na virusi vya ukimwi lakini wanasema ni nusu tu ya idadi hiyo ndio wanaopokea matibabu.

Moja ya sababu inayotajwa kuleta ugumu kwa watoto wadogo kunywa dawa za virusi vya ukimwi ni ladha yake chungu.

Wataalamu wa Afya wanasema sasa hatua ya kusaidia kukabiliana na hali hiyo inawadia dawa zenye ladha tamu zitakuwa muafaka kabisa kwa watoto wenye VVU.

Na pia hatua hiyo inamaanisha hakutakuwa na haja ya kuvunja mara mbili dawa za watu wazima kwa ajili ya watoto.

DPP: Hii ndio sababu ya kumuachia huru Nusrat Hanje
Azam FC yawatumia salamu Gwambina FC