Watanzania wametakiwa kuacha tabia ya kutumia dawa za kutuliza maumivu mara kwa mara bila kushauriwa na daktari, kwani ni chanzo cha tatizo la figo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile ametoa ushauri huo leo jijini Dodoma katika maadhimisho ya siku ya Figo Duniani.

“Unaweza kukuta mtu amechoka ametembea siku nzima anaenda kununua dawa ya kutuliza maumivu anameza na maumivu yanatulia, wakati alitakiwa kupumzika na kunywa maji mengi tu,” IPP wanamkariri Dkt. Ndugulile ambaye ameeleza kuwa magonjwa ya figo yameongezeka nchini.

Leo, dunia nzima inaadhimisha ugonjwa wa figo ambapo madaktari na watalaam wa afya wamejitokeza kutoa elimu kuhusu matatizo hayo kama hatua ya kusaidia kuyatokomeza.

Mtandao wa NDTV umeandika makala ya kitabibu inayoonesha kuwa ulaji wa vyakula vyenye protini kupita kiasi pia ni chanzo cha tatizo la figo.

“Ulaji wa vyakula vyenye protini kupita kiasi unaweza kuathiri afya ya figo lako mbali na faida nyingi zinazotokana na vyakula hivyo,” wameandika.

Katika makala hiyo iliyoandikwa na mtaalam wa afya, Mansha Dhingra , wamewashauri watu wanaotaka kutengeneza miili ikiwa ni pamoja na kupungua kwa kutumia milo ya protini kuhakikisha wanapata ushauri wa kitabibu kabla ya kuanza zoezi hilo.

Spika Ndugai amshangaa Lissu,' Huwezi kudai mshahara mitandaoni'
Ethiopia yavipeleka Ufaransa visanduku vya kurekodi ndani ya Ndege

Comments

comments