Shirika la Maji Safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) limetangaza kuzima mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu kwa saa 14 kesho Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa tano usiku.

 

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari  na Ofisi ya Mahusiano yaShirika hilo leo  jijini Dar es Salaam inaeleza kuwa sababu kuu ya kuzimwa kwa mtambo huo ni kuruhusu usafishaji wa bomba jipya na kufanya majaribio ya sehemu ya mtambo mpya wa Maji wa Ruvu juu.

 

Pia zoezi hili linahashiria hatua za mwisho za mtambo huo kukamilika na kuanza kutumika ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo.

 

Maeneo ambayo yatakosa maji ni Mlandizi Mjini , Ruvu darajani, Vikuruti, Disunyara, Kilangalanga, Janga, Mbagala, Visiga, Lulinzi, Kibamba, Kibamba njia panda, Shule kibwegere, Mloganzira, Kwembe, Kibamba hospital, Kwa mkinga, Luguruni ,Maili 35, Zogowale, Misugusu,Tanita, Kibondeni, Kwa mathias, Nyumbu, Msangani, Kwa mbonde, Picha ya Ndege, Sofu na Gogoni.

 

Pia zoezi hili linahashiria hatua za mwisho za mtambo huo kukamilika na kuanza kutumika ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo.

 

Aidha Shirika linatoa ushauri kwa  wananchi  kuhifadhi maji na kuyatumia kwa matumizi ya lazima

Tibaigana Afunguka Kuhusu Maandamano Ya Vyama Vya Siasa
Rais Magufuli Awataka Wahandisi Kufanya Kazi Kwa Weledi