Mtayarishaji wa muziki, Daxo Chali ameachana na wasanii wake wawili wa kike, Nini na Haithan waliokuwa wakifanya kazi chini ya usimamizi wake, baada ya kubaini kuwa mmoja ana uhusiano ya kimapenzi na Nay wa Mitego.

Akizungumza na EATV, Mtayarishaji huyo amesema kuwa Nini ni msichana mdogo hivyo anaona kujihusisha kimapenzi na Ney wa mitego kunaharibu ‘brand’ aliyokuwa anahangaika kuitengeneza.

“Mimi nilishtuka kuona Nini ambaye ana miaka 18… Ney wa Mitego wa nini tena!? Alihoji. “Mimi nimeshtuka watu wengine wamatuchukulia kawaida. Mara ya kwanza nilipotezea lakini baada ya muda wasanii wakubwa wakawa wananiletea ‘mbona yule dogo nakutana nae hivi mara vile..?’” aliongeza.

Daxo amesema kuwa amekuwa akiwakanya wasanii hao mara kwa mara lakini hawakumsikiliza hivyo ameamua kubwaga manyanga.

Hata hivyo, amesema kuwa kwa muda ambao amefanya kazi na wasanii hao amegundua wana vipaji vya kipekee, hivyo anawaombea mafanikio katika kazi zao za muziki.

Daxo ambaye ni mdogo wa mtayarishaji nguli, Marco Chali ni moja kati ya watayarishaji wakubwa kutoka katika familia hiyo. Watayarishaji wengine kutoka katika familia hiyo ni Beef Chali na Zacha wote wakifanya kazi ndani ya MJ Records.

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 30, 2017
Rais wa Iran ashikilia msimamo wake juu ya utengenezaji wa silaha