Mwimbaji Dayna Nyange huenda leo angekuwa miongoni mwa rappers wakali wa kike kwenye historia ya muziki Tanzania kabla hajageukia upande wa pili wa shilingi.

Dayna Nyange ambaye wimbo wake wa ‘Mafungu ya Nyanya’ akiwa na Marlaw ulimtambulisha kwa nguvu zaidi kwenye tasnia ya muziki nchini amesimulia maisha yake kabla ya uimbaji na kueleza kuwa alikuwa rapa mkali kiasi cha kuligusa sikio la mmiliki wa studio za B’Hitz, mtayarishaji mkali wa muziki, Hermes Joachim aka Hermy B aliyetaka kumsaini kwenye lebel hiyo.

Kumbuka Hermy B ni moja kati ya majaji wa shindano la kusaka vipaji la ‘Tusker Project Fame’ hivyo kulikuna sikio lake kwa rap lazima uwe na uwezo mkubwa.

Hermy B (kulia), akiwa na Jaji Ian na Juliana Kanyomozi katika Shindano la Tusker Project Firms

Hermy B (kulia), akiwa na Jaji Ian na Juliana Kanyomozi katika Shindano la Tusker Project Fame

Dayna aliuambia mtandao wa Bongo5 kuwa yeye alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kutaka kusainiwa na B’Hitz kama rapa wakati inamsaini pia mtayarishaji wa muziki, Pancho Latino ambaye baada ya muda mfupi alionesha uhodari mkubwa wa kutayarisha midundo ya ngoma kubwa.

Amesema kuwa muda wa kusubiri pamoja na umbali (alikuwa anaishi Morogoro) vilikuwa kikwazo kwake kuendelea kuwa karibu na B’Hitz na hatimaye kuachana nao kabisa.

“Halafu na mimi nilikuwa ni mtu mwenye misimamo fulani… unajua hip hop nazo huwa zinatuharibu wadada, ‘mbona mimi bado mkali sana halafu kama wananiwekaweka, au kwa kuwa mimi ni mnyonge au wananichukuliaje,” alisimulia.

“Ilikuwa kipindi kile nilikuwa nachukuliwa mimi alikuwa anachukuliwa na Pancho, kwahiyo walikuwa wanatuangalia kama mimi naweza kuingia moja kwa moja kwenye label au vipi. Pancho kwa sababu alikuwa yuko Dar aliweza kuwa nao karibu mpaka akaenda. Mimi nilikuwa nashindwa kwa sababu nilikuw bado niko Morogoro kwahiyo kama ni wiki ilitakiwa nije nikae huku Dar,”aliendela kusimulia.

Anasema kuwa umbali ulimkatisha tamaa na kuwaweka mbali na B’Hitz na baadae alibadili muelekeo na kuanza kuimba na kufanikiwa kusikika na kukubalika.

Hivi sasa, Dayna ameachia wimbo wake mpya pamoja na video alioupa jina la ‘Angejua’.

Mrema apigwa chini Mahakamani, Akubali Kumlipa Mbatia
Mapenzi: Sehemu 4 za mwili usizopaswa kumshika mkeo nyakati hizi 18+