Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaj Majid Mwanga ameibuka mshindi wa nafasi ya Kwanza akichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa kwa kupata kura 1,202 kati ya 1,562 zilizopigwa huku akiwaambia wajumbe kwa utani leo watu ni wapole.
Uchaguzi huo, ulikua na wagombea 12 (walio wania nafasi ya uwakilishi mkutano mkuu taifa), huku washindi watatu wa juu wakipata nafasi hiyo, ambapo kati ya kura 1562 zilizopigwa, 149 ziliharika, Sabina Kinyowa akipata kura 652 na Dkt. Chisuligwe Salum akiwa na kura 543.
Baaada ya ushindi huo, DC Mwanga amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu Wilaya na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi wengine wa Chama na Serikali .
Katika uchaguzi huo, Amer Mbarack amefanikiwa kukitetea kiti chake cha uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya baada ya kuibuka na kura 1,212 dhidi ya mshindani wake liyepata kura 341.