Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaji Majid Mwanga amewajia juu baadhi ya waamuzi wa mchezo wa Soka wa wilaya yake na kuwataka kuacha mara moja kumfanyia visa na vitimbi katika utekelezaji wa majukumu yake, huku akiwasii kujenga uhusiano mzuri miongoni mwao.
 
Ukweli huo mchungu ameutoa wakati wa mkutano Mkuu wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Pwani,  akiwa mgeni rasmi.
 
Mkutano huo umeshirikisha waamuzi na viongozi wa vilabu vya wilaya Saba za Mkoa wa Pwani. Katika mkutano huo mkuu huyo wa wilaya baada ya kusikia changamoto wanazokabiliana nazo Chama hicho cha soka mkoa, ameahidi kuchangia shilingi milioni moja.
Amemtaka mwenyekiti wa Chama cha Mpira Mkoa wa Pwani, Hassan Hasanoo kurekebisha kasoro zilizopo kati yake na waamuzi hao ili mchezo huo uendeshwe kwa mafanikio suala ambalo, Hassanoo amemuhakikishia mkuu huyo wa wilaya kulichukulia hatua na kuhakikisha uhusiano mzuri baina yao unakuwepo.
 
Hassanoo pia amewaomba wajumbe kuzikubali fedha hizo ili kuipa nguvu Timu ya Kiluvya United ili iweze kutatua changamoto zake.
Rais Karia Ashinda Ujumbe CECAFA
Video: GSM yazindua promosheni mpya