Mkuu wa Wilaya ya Kinondini, Ally Hapi amesema kuwa atawafutia leseni wamiliki wa hoteli na kampuni binafsi ambao hawajatoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao ambao wamekuwa wakifanya kazi katika makampuni hayo.

Ameyasema hayo wakati wa ziara wilayani humo ya kutembelea baadhi ya hoteli na kampuni binafsi kwa lengo la kuzungumza na wafanyakazi ambao wamekuwa wakilalamika kuhusu kutopata mikataba.

Aidha, wafanyakazi walilalamikia mazingira magumu ya kazi ikiwamo mishahara duni na kufanya kazi bila mikataba.

Vile vile afanyakazi mbalimbali katika ziara hiyo wamesema kuwa licha ya kufanya kazi kwa miaka mitano, hawajawahi kupatiwa mikataba huku wakinyimwa stahiki ikiwamo likizo na matibabu.

Hata hivyo, baadhi ya wamiliki wa hoteli na makampuni mbalimbali ya binafsi wamekiri kutotoa mikataba tangu waanze kufanya kazi katika makampuni hayo na hoteli lakini wameanza utekelezaji wiki hii.

Argentina, Uruguay kuandaa kombe la dunia 2030
Mpenzi wa muuaji wa Las Vegas afunguka, 'nilipata wasiwasi'