Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewaagiza Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Sheila Edward kuleta Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza Mradi wa Upimaji ardhi uliosimamiwa na Uongozi wa kata awamu iliopita.
“Katibu Tawala Ilala nakuagiza ulete TAKUKURU waje kuchunguza katika kamati ya Mradi wa Upimaji Kama kuna rushwa imetumika taasisi itafanya kazi yake'” amaesema Mjema.
Mjema alitoa agizo hilo katika mwendelezo wa ziara ya siku ya pili Kata ya Kipunguni wakati akijibu kero za wananchi wakidai fedha iliyotumika katika urasimishaji makazi ya Upimaji imevuka kiwango cha Serikali kutoka shilingi 250,000 mpaka kufikia sh, 460,000 kwa Kata ya Kipunguni.
Amesema Serikali ya Rais John Magufuli ni sikivu haki itatendeka na kama ndani Kamati ya Upimaji mkono wa rushwa umetumika wote waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Sophia Mjema alisema dhumuni ya ziara yake kuzindua miradi na kutatua kero za wananchi wa wilaya ya Ilala mara baada kumaliza ziara katika Jimbo La Ukonga, ziara itamia Jimbo la Segerea.
Kwa upande wake Mwananchi wa Kipingu Sakina Yusuph alisema katika kata hiyo Mradi wa Upimaji ulianza mwaka 2012 ambapo kila Mwananchi ametozwa shilingi 460,000 shilingi 50,000 waliambiwa ya Upimaji na shilingi 410,000 ya mpima lakini mpaka sasa wengine hawajapimiwa.
Akijibu tuhuma hizo aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo Nyasika Getama alisema katika Mradi huo wa wakazi waliolipa fedha hizo baadhi wameshapimiwa na wengine wameshindwa kupimiwa kutokana na kuwa katika maeneo yaliotengwa kwa Viwanda
Nyasika aliwataka wananchi wasimdanganye Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa kumpa maelezo ya uongo.
‘”Mradi huu ulikuwa katika uongozi wangu wa udiwani nilivyomaliza udiwani, Diwani mwenzangu mpya Mohamed Msophe yeye hausiki hivyo alinipa ridhaa nimalizie kusumamia Mpango huo.
Kwa upande wake ofisi Ardhi wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela amesema uongozi wa mtaa wamepewa jukumu la kukaa kikao na wananchi kwa ajili ya kukubaliana kurasimisha makazi mara baada kukubaliana gharama za kulipia mpima shilingi 250,000 viwango vya Serikali ambavyo vimetangazwa na Waziri William Lukuvi.
Amesema Kama aridhi ilipangwa kwa matumizi mengine aidha viwanda au vituo vya afya mwenye mamlaka ya kubadilisha matumizi ya ardhi ni Serikali sio mwananchi na Serikali inabadilisha matumizi bila fedha yoyote hivyo wananchi wasidanganyike kutoa fedha katika hilo la kubadilisha matumizi ya ardhi ya Serikali.
Wakati huohuo Mwananchi Sakina Yusuph ametangaza kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi cha Kata Kipunguni kwa ili kuimalisha ulinzi kwa wananchi.