Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo leo Septemba 19 amezindua rasmi kampeni ya ‘Tokomeza zero’ inayolenga kuwasaidia wanafunzi wa Wilaya ya Kisarawe kwa kuwaandalia mazingira mazuri ya kujifunzia ili kuhakikisha wanatokomeza idadi kubwa ya wanafunzi wanaofeli.

Kupitia kampeni ya ‘Tokomeza Zero’ yenye malengo ya kukusanya michango mbalimbali ili kuweza kusaidia gharama mbalimbali za mahitaji ya kuboresha elimu amealika wadau mbalimbali kutoka sekta mbalimbali kufanikisha lengo hilo.

DC Jokate amesema mahitaji yanayohitajika ni pamoja na miundombinu, ikiwa ni pamoja na meza 484 na viti 642, matundu ya vyoo 113, ofisi za walimu, makatba 13, mabweni, madarasa 68 ambapo makadirio ya mkakati ya muda mrefu ni shilingi bilioni 4.1.

Hivyo, amewaomba wananchi wa Tanzania pamoja na wadau mbalimbali kuchangia kiasi chochote cha pesa kwa simu zao za mkononi kupitia 0657  855 359 kwa jina la Ondoa  Zero Kisarawe au kupitia akaunti maalumu ya kisarawe ya ”Development Fund” ya NMB kwa namba 21410009647.

Ameongezea kuwa kwa yeyote mwenye chochote anaweza kuchangia kama ni kujenga madarasa, au kuchangia vyakula shuleni anakaribishwa lengo ikiwa ni kuboresha miundombinu na kuwasaidia wanafunzi katika ufaulu kwa kuwawekea mazingira rafiki.

Aidha, amewaalika waandishi wa habari katika harambee inayotarajiwa kufanyika Septemba 22, 2018 majira ya saa 5 asubuhi katika ukumbi wa shule ya Sekondari Minaki inayotarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali kama vile wasanii na wadau mbalimbali wa elimu.

 

Video: Haya ndiyo maisha halisi ya Hamissa? 'Madam Hero'
LIVE: DC Jokate anaongea na waandishi wa habari muda huu. Tazama