Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amefanya oparesheni ya kuwaondoa wakulima na wafugaji waliovamia Msitu wa Ruvu Kusini na kukamatwa Ng’ombe zaidi ya 150.
Amefanya ziara hiyo ikiwa ni siku kumi tangu kuteuliwa kwake, ambapo amesema kuwa lengo la oparesheni hiyo ni kutekeleza sheria ya misitu ya mwaka 2002, inayosema hairuhusiwi shughuli zozote za kijamii na kiuchumi kufanyika katika eneo la hifadhi.
“Leo tumefanya oparesheni hii katika Msitu wa Ruvu Kusini, nitoe rai kwa wananchi wa Kisarawe kwani hatutamvumilia mtu atakayekaidi agizo la kusitisha shughuli za kilimo na ufugaji msituni,” amesema Jokate.
Aidha, Julai 28, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa Mikoa, Wizara na Wilaya, ambapo Jokate aliteuliwa kuiongoza Wilaya ya Kisarawe.
-
Dkt. Kalemani apiga marufuku TANESCO, REA kuagiza vifaa nje ya nchi
-
Video: Polisi feki wakamatwa Jijini Dodoma wakikusanya mapato
-
NEC yavitahadharisha vyama vya siasa vitakavyokiuka utaratibu
Hata hivyo, Jokate aliapishwa na kukabidhiwa Ofisi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, tarehe 3, Agosti ambapo baada ya kiapo alisema kuwa anadeni kubwa kwa Rais baada ya kumteua na atahakikisha anafanyia kazi maagizo aliyopewa.