Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela ameongoza oparesheni ya kuwasaka wafanyabiashara wasiotumia risiti za mashine (EFD) katika maduka mbalimbali ya manispaa ya Iringa.
 
Katika oparesheni hiyo iliyofanywa katika eneo la Miyomboni ilihusisha wafanyabiashara wa maduka mbalimbali ambapo wengi wao wamekutwa na makosa ya kutotumia mashine hizo.
 
Akizungumza mara baada ya oparesheni hiyo, Kasesela amewataka wafabiashara kutumia mashine za kutolea risiti kila wanapouza bidhaa zao na jamii kudai risiti kila wakati baada ya kubaini asilimia kubwa hawatumii EFD mara kwa mara..
 
Amesema kuwa serikali inawategemea sana wafanyabiashara kulipa kodi lakini serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara wasiolipa kodi zao kwani wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
 
Kwa upande wake Meneja mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa, Lampson Tulianje amesema kuwa wafanyabiashara wa wengi wana mwitikio mdogo wa kutoa risiti za EFD baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali.
 
  • Bob Chacha Wangwe ahukumiwa kwenda jela
 
  • Video: Rais Magufuli siyo wamchezo mchezo, Mwisho wa enzi za Mugabe
 
  • Kamati ya Bunge yawaweka kitimoto waandishi wa habari
 
Hata hivyo, ameongeza kuwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao pasipo kuwapatia risiti za mashine za Kielektroniki (Efd) wateja wao mara kwa mara hali inayokosesha TRA mapato hivyo pindi watakapobainika watafikishwa katika vyombo vya sheria na kuchukua mali zao hadi wamalizapo
Tume ya uchaguzi yapokea taarifa kutoka kwa Spika Ndugai
Kama ulituma Waraka huu imekula kwako