Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Shamwengo kata ya Inyala halmashauri ya wilaya mbeya na kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzipatia majibu yake.

Katika mkutano huo, Malisa aliambata na Mwenyeliti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Mwalingo Kisemba, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Stephen Katemba pamoja na wataalam mbalimbali.

Pamoja na mambo mengine, Malisa pia amewahamasisha wananchi hao kujitokeza kwa wingi siku ya mkesha wa mwenge wa uhuru unaotarajia kufika Semptember 10 mwaka huu na kukesha katika kijiji cha Inyala.

Hata hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Stephen Edward Katemba amewahakikishiwa wananchi hao kuwa Zahanati ya shamwengo itaanza kazi rasmi na kwamba kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji imeanza kushughulikiwa.

Bayern Munich yapiga hatua kwa Harry Kane
Chama: Miquissone alitamani kurudi Simba SC