Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewatoa hofu wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Juu ya Changamoto ya kutokuwepo kwa huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo katika Halmashauri hiyo na ubovu wa miundombinu ya Barabara Katika maeneo machache.

Malisa ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara ulioambatana na ukaguzi wa kituo cha afya Cha Mbalizi katika kata ya Utengule iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ambapo wakazi wa eneo hilo wamebainisha kero hizo na kuomba Serikali kuzitatua.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.

Amesema, Mkandarasi wa mradi mkubwa wa Barabara ya njia nne ameshaweka kambi tayari kwa ujenzi utakao ondoa shida ya foleni kuanzia jiji la Mbeya hadi Uwanja wa ndege wa Songwe, kwani mradi huo wa Kimkakati utapita Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Aidha, Malisa pia amewataka wananchi hao kuwa na uvumilivu kwani Serikali Inaendelea na taratibu za Kutatua kero ya maji Mkoani Mbeya na tayari mkataba wa mradi wa Maji wa Mto Kiwira umesainiwa na unatarajia kuwanufaisha wakazi wa Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake.

Kilimo waomba kuidhinishiwa zaidi ya Bilioni 970
Mo Salah afikia rekodi ya Steven Gerrard