Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri amewaagiza watumishi na wakuu wa idara kuacha uvivu wa kuagiza barua zinazohitaji utekelezaji wa haraka katika ofisi zilizopo karibu na maeneo yao badala yake waweze kwenda nazo mikononi ili kupata majibu ya utekelezaji kwa wakati.

Ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha baraza la madiwani ambapo ameagiza kuwa barua zilizopo katika ofisi jirani na ofisi zingine ni lazima zipelekwe kwa mkono na si kwa barua pepe.

“Niseme tu kwamba kuna mambo mengine yanatuchelewesha sana sasa unakuta ofisi iko karibu tu halafu tunatuma watu kupeleka barua na tunaanza kuuliza barua imefika, huku nikuchelewesha muda na wakati mwingine mpaka tunafuatilia wiki hadi mwezi, tubadilike watendaji, hatuwezi kufika tunachelewa kwa kujichelewesha,”amesema DC Msafiri

Aidha, mkuu huyo wa wilaya amesisitiza kufuatilia maendeleo ya mazao mkakati hususani zao la Chai ambalo linaendelea vizuri katika wilaya ya Njombe.

Hata hivyo, katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewaagiza madiwani kuhakikisha wanasimamia zoezi la wanafunzi waliofaulu kuendelea na elimu ya Sekondari na wanajiunga kwa wakati.

 

Mtangazaji asukumwa ndani baada ya kufanya mahojiano na Shoga
Tril. 1.5 zazua mjadala mkubwa, 'Kama akithibitisha niko tayari kuhamia CCM'- Ado Shaibu

Comments

comments