Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ameamuru kukamatwa na kuwekwa rumande kwa saa 48 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tudi inayomiliki Shamba la Kibo and Kikafu Estate ,Jensen Natal pamoja na Manasheria wa kampuni hiyo, Edward Mroso.
Â
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameamuru kushikiliwa kwa muda Pasi ya kusafiria ya anayetajwa kuwa mwekezaji wa Shamba la Kibo and Kikau Estate,Trevor Robert kutokana na tuhuma za kukwepa kulipa kodi ya serikali inayokadiliwa kuwa zaidi ya Shil. Mil 700