Mkuu wa Wilaya ya Rorya Simon Odunga amepiga marufuku ya uchomaji mkaa na kuwaonya wazazi wanaotumikisha watoto katika shughuli hizo za uchomaji mkaa.

Odunga ametoa agizo hilo kama mkakati maalum wa utunzaji mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala.

Aidha, Odunga amesema kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria na kuwaasa kupanda miti na kuepukana ukataji miti holela.

Maofisa Kilimo wa Kata wilayani humoo wametakiwa kuwaelekeza wananchi katika maeneo yao kufanya kilimo bora cha mazao ya chakula na biashara yaliyo rafiki kwa mazingira na kuepuka kukata miti ya asili.

Simba SC kuangukia kwa TP Mazembe, Zamalek, Kaizer Chief
Uganda yapiga marufuku simu katika uchaguzi