Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Lazaro Twange na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati, Pendo Mangali wamefanya ziara ya kutembelea wawekezaji wa ndani kwa lengo la kutatua changamoto ili kuweza kuongeza nguvu ya ajira kwa Vijana na kupunguza urasimu wa ufanyaji Biashara na Uwekezaji.

Wameyazungumza hayo katika eneo la Viwanda na kuongeza kuwa pia Wawekezaji wote wanatakiwa kutekeleza maagizo waliyopewa na Serikali, ili kuweza kutoa ajira kwa Vijana wengi.

‘’Tuna wajibu wa kuziwezesha sekta binafsi ili ziendelee kwasababu kanuni sheria na taratibu sisi ndio tunazisimamia serikali ya awamu ya sita inasisitiza kupunguza urasimu kwenye ufanyaji biashara ndio maana tunakuwa na mabaraza ya biashara,” alisema DC Twange.

Aidha, ameongeza kuwa, “lakini tumekuja kuwatembelea ili kusikia serikali inaweza kufanya hii ndio kazi ya serikali kuhakikisha inapunguza mnyororo wa hatua zisizokuwa za lazima zinazosababisha biashara isifanyike kwa kasi inayo stahili.’’

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Pendo Mangali amesema, “yale yote mliyoelekezwa na Mkuu wa Wilaya kuhusu namna bora ya kuboresha biashara, pia Vijana waliowaajiri wanaonekana ni wadogowadogo na tunashukuru kwa hilo mmeweza kutusaidia lakini pia yale yote mliyoahidi wekeni vizuri ili kazi iendelee kuwa nzuri Zaidi.’’

Naye meneja wa Dutchkon limited, Norvart amesema “kwa yale ambayo mmetuasa tutaenda kuyafanyia kazi haraka tunaendelea na upanuzi wa kiwanda chetu tunajenga kiwanda kingine ili tuweze kutoa ajira nyingi Zaidi na tuwezekufanya uzalishaji mkubwa Zaidi ya huu wa sasa.’’

Elimu ya lazima kuwa miaka 10 - Waziri Mkuu
Deschamps: Ronaldo, Mbappe ni zaidi ya Messi