Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Kupambana na Dawa za Kulevya – DCEA, kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama imefanya operesheni ya siku nane Mkoani Morogoro na kukamata Magunia 131 za bangi kavu iliyotayari kusafirishwa, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketeza jumla ya hekari 489 ya mashamba ya bangi na Watuhumiwa 18 kukamatwa.

Katika Wilaya ya Morogoro Vijijini kata ya Kisaki, Kijiji cha Rumba zilikamatwa gunia 70 za bangi, Kijiji cha Mbakana zimekamatwa gunia 59 za bangi, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketezwa hekari 350 za mashamba ya bangi. Aidha, wilayani Mvomero Mamlaka imeteketeza hekari 139 na wilaya ya Morogoro zimekamatwa gunia mbili (2) za bangi.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema wakulima wa bangi Mkoani Morogoro wamekuwa wakichepusha Maji pembezoni mwa mto na kukata miti, ili waweze kupata maeneo ya kulima bangi.

Amesema, “wanachepusha maji na kuyazuia yasiende kwenye maeneo mengine yakahudumie wananchi kumwagilia mashamba yao, wanafanya uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti katikati ya msitu ili walime bangi,” amesema Lyimo.

Aidha, ameesema “niwaase wananchi wote watusaidie kutoa taarifa za wakulima wa bangi na mirungi katika maeneo mbalimbali, ili tuwakamate na kuharibu mashamba yao. Kwani mbali na madhara mengine yanayotokana na zao la bangi, wakulima hawa wanaharibu misitu, vyanzo vya maji.”

Try Again: Tutarudisha heshima yetu 2023/24
Harry Kane anasubiri muda wa kuondoka