Kiungo kutoka nchini Ujerumani Julian Draxler, hatimae ameachana na klabu ya Schalke 04 na kujiunga na klabu ya VfL Wolfsburg kwa mkataba wa miaka mitano.

Kiasi cha Euro million 35 kimetajwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchini Ujerumani katika usajili wa Draxler, ambaye alipigiwa upatu wa kuelekea nchini Italia kujiunga na klabu bingwa nchini humo Juventus siku kadhaa zilizopita.

Usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 kuelekea VfL Wolfsburg umechangiwa na hatua ya kuundoka kwa kiungo kutoka nchini Ubelgiji Kevin De Bruyne ambaye amekamilisha mpango wa kujiunga na Man City ya nchini England.

Wolfsburg, wametumia kiasi cha fedha walizozipata wakati wa dili la kuuzwa kwa De Bruyne, kumsajili Draxler, na pia amefanikiwa kumsabili beki kutoka nchini Brazil na klabu ya Bayern Munich  Dante.

Klabu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye ligi ya nchini Ujerumani msimu uliopita, ilitunisha mfuko wake kimapato kwa kumuuza De Bruyne, Euro million 75.

Draxler, ameondoka Veltins-Arena, Gelsenkirchen baada ya kushuhudia akiitumikia Schalke 04, kwa muda wa miaka 14.

Draxler, alijiunga na kikosi cha vijana cha klabu ya Schalke mwaka 2000 akitokea kwenye kituo cha vijana cha SSV Buer 07/28, na alipowasili mjini Gelsenkirchen alionyesha uwezo mkubwa na hatimaye alipandishwa kwenye kikosi cha wakubwa mwaka 2011, alipokuana umri wa miaka 17 ambapo alicheza michezo 119 na kufunga mabao 18.

Jokate Aja Na Kitu Kipya
Watuhumiwa Wizi Akaunti Ya EPA Waachiwa Huru