Kuna uwezekano mkubwa kwa timu ya A-Etifag ya Saudi Arabia ikawasilisha ofa ya kuwasajili kwa pamoja Kevin de Bruyne wa Man City na Victor Osimhen wa SSC Napoli katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya baridi.

Taarifa hii imeibuka baada ya kocha wa wababe hao, Steven Gerrard kuthibitisha kwamba timu hiyo imepanga kuingia sokoni Januari 2024, kwa ajili ya kusajili mastaa mbalimbali kutoka Barani Ulaya.

Katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi A-Etifaq ilifanikiwa kuwasajili Jordan Henderson, Georginio Wijnaldum na Damarai Gray, lakini bado inataka kuendelea kumwaga mkwanja kwa ajili ya kunasa mastaa wengine.

Osimhen ambaye mkataba wake unamalizika 2025, aliwahi kuhusishwa na baadhi ya timu za Saudia Arabia katika dirisha lililopita la kiangazi, lakini mchakato ulishindikana.

Kwa upande wake De Bruyne, Manchester City inadaiwa kutohitaji kumsainisha mkataba mpya kutokana na hali yake ya majeraha ya mara kwa mara yanayomsumbua kwa sasa.

Mashujaa FC wanalitaka dirisha dogo
Maxi Nzengeli afichua siri ya mafanikio