Mlinda mlango wa Manchester United, David De Gea amepasua ukweli wa mambo yanavyoendeshwa kwenye klabu hiyo kufuatia kuachwa kwake nje katika mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Spurs, ambapo The Red Devil waliibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

De Gea amepasua ukweli huo baada ya kuthibitika hatokuwepo tena langoni kwa mara ya pili hii leo, katika mchezo mwingine wa ligi ya nchini England, ambapo Man Utd watafunga safari kuelekea mjini Birmingham kupambana na Aston Villa kwenye uwanja wa Villa Park.

Mlinda mlango huyo amesema maamuzi ya kuwekwa nje ya kikosi cha kwanza ameyaafiki na alikua chanzo cha yote yaliyotokea tangu mwishoni mwa juma lililopita, kwa kusudio la kutaka kujua hatma yake hadi siku ya mwisho ya usajili huko barani Ulaya.

Amesema kabla ya kuwekwa nje katika mchezo wa kwanza, alikua na mazungumzo na kocha wa makipa klabuni hapo Frans Hoek na alimthibitishia kutokua tayari kukaa langoni kutokana na hali yake ambayo imekua ikihusishwa na msongo wa mawazo ya kutaka kuhamia kwenye klabu ya Real Madrid.

Mlinda mlango kutoka nchini Argentina, Sergio Romero alianza katika mchezo huo walioshinda dhidi ya Tottenham nah ii leo anatarajiwa kukaa langoni kwa mara ya pili kwenye mpambano dhidi ya Aston Villa.

Arsenal Wapata Ahuweni
CNN Wajishusha kwa Rais Kenyatta Baada Ya Kuwashukia