Mlinda mlango wa klabu ya Man Utd, David De Gea atakuwa sehemu ya wachezaji wa klabu hiyo watakaoanza mazoezi hii leo ya kujiwinda na msimu mpya wa ligi ya Uingereza.

De Gea, anatarajiwa kuanza mazoezi na kikosi cha Man Utd ikiwa ni baada ya siku kadhaa kuonekana mjini Madrid ambapo uvumi uliendelea kudai kwamba mipango ya kutaka kujiunga na klabu ya Real Madrid ilikua inaelekea ukiongoni.

Kati kati ya juma lililopita Meneja wa man Utd alimtaka kipa huyo chaguo la kwanza la Man utd kufika mazoezini bila kukosa mwanzoni mwa juma hili, hali ambayo itatimizwa hii leo.

Hata hivyo kituo cha televisheni cha mjini Madrid kiitwacho Cuatro, kimeripoti kwamba pamoja na matarajio ba De Gea kuwa sehemu ya kikosi cha Man utd kitakachoanza mazoezi hii leo, bado viongozi wa Real Madrid hawajakata tama ya kumsajili katika kipindi hiki cha majira ta kiangazi.

David De Gea amekua gumzo la kutaka kusajiliwa na klabu ya Real Madrid kwa kipindi kirefu, kufuatia mlinda mlango wa sasa wa klabu hiyo Iker Casillas Fernández kuonekana uwezo wake unazidi kuporomoka siku hadi siku.

Silaha Za Azam Toka Ughaibuni Zajiandaa na Kagame Cup
Riquelme: Nilifanya Makosa Makubwa Kuikataa Ofa Ya Man Utd