Harakati za mlinda mnlango David De Gea za kutaka kurejea nyumbani nchini Hispania na kujiunga na klabu ya Real Madrid, huenda zikagonga mwamba kufuatia uzembe ambao umeripotiwa kufanywa na viongozi wa klabu hiyo ya mjini Madrid.

De gea yupo njiani kurejea nyumbani Hispania kwa ada ya uhamisho wa paund million 29, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili usiku wa hii leo.

Taarifa kutoka Old Trafford zinaeleza kwamba, mpaka sasa kuna baadhi ya karartasi za usaijili wa mlinda mlango huyo (paperwork), hazijawasilishwa na tayari wasiwasi umeanza kuibuka miongoni mwa viongozi wa Man Utd kama wataweza kufanikisha usajili wa De Gea ambaye anatarajiwa kuwa mrithi wa Iker Cassillas.

Hata hivyo taarifa hizo hazijathibitishwa rasmi na uongozi wa Man Utd, na badala yake zimekua zikitolewa kama tetesi kufuatia baadhi ya mambo kuonekana kukwama tangu jana.

Inadaiwa kwamba Real Madrid wamekubali kutoa fedha pamoja na kumuachia mlinda mlango wao kwa sasa Keylor Navas, ili kukamilisha dili la kumsajili De Gea.

Januzaj Apigwa Bei Ujerumani
Moses Kuihama Chelsea Leo