Meneja wa muda wa Klabu ya Leicester City, Dean Smith anaamini watarejea tena Ligi Kuu England baada ya kushuka daraja licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United katika mechi ya mwisho ya ligi juzi Jumapili (Mei 28).

Leicester iliiombea mabaya Everton ipoteze mechi yao hata hivyo ikaibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bournemouth na ikaepuka kushuka daraja.

Ikumbukwe Leicester imeshuka daraja kwa mara ya kwanza baada ya miaka saba ilipobeba ubingwa wa Ligi Kuu England, hata hivyo Smith akasisitiza watarejea tu.

Leicester itacheza Championship msimu ujao baada ya Everton kujikomboa kwa sababu ushindi wa mabao 2-1 haukuwa wa maana kwa upande wao.

Smith amedai baada ya msimu kumalizika ataongea na mwenyekiti wa klabu Aiyawatt Srivaddhanaprabha, ambaye atapanga mikakati mizito baada yab kufanya vibaya msimu huu.

“Leicester ni klabu kubwa England, inauma sana kwa hapa ilipofikia, kila mtu amevurugwa lakini kutokana na mipango mizuri inayokuja kwa ajili ya timu naamini itarejea Ligi Kuu, kuna wakati timu lazima itapitia kipindi kigumu, kwa hiyo kazi kubwa inayofuata ni kurudi kwa kishindo,”

“Sina mashaka na hii klabu inaweza, nadhani ni kujipanga tu kutokana na yaliyotokea, nitaongea na mabosi mambo kadhaa kwa sababu naheshimiana nao, tutazungumza mengi kuhusu klabu kwani nguvu inahitajika zaidi na muda pia” amesema Smith

Kufuatia Leicester kushuka daraja msimu huu huenda ikawapoteza mastaa wao kama James Maddison anayewindwa na klabu kubwa kama Manchester United, Chelsea na Arsenal.

Leciester City iliuanza msimu wa 2022-2023 bila ya kufanya usajili wa nguvu huku Brendan Rodgers akifukuzwa kutokana na matoke mabovu nafasi yake ikachukuliwa na Smith.

Ukiifanyia mabadiliko Gari yako unaweza usilipwe Bima - RSA
Mauricio Pochettino aonywa mapema Chelsea