Klabu ya Arsenal imemsajili Kiungo kutoka England Declan Rice na itakuwa na matumaini kwamba imeboresha safu yake ya kiungo.

Mchezaji mwenye umri wa miaka 24, anatarajiwa atafanya mambo makubwa, kutokana na takwimu zake za Ligi Kuu kwa msimu uliopita akiwa na The Hummers.

Nahodha huyo wa zamani wa West Ham anafanya vyema katika eneo moja maalumu ikilinganishwa na viungo wengine wa Arsenal.

Rice ana uwezo wa kuingia na mipira katikati ya dimba zaidi kuliko Martin Odegaard, Jorginho, Thomas Partey na Granit Xhaka, ambaye sasa yuko Bayer Leverkusen.

Kiungo huyo aliingia na mipira eneo la dimba la kati mara 63, zaidi ya Partey, ambaye aliyeingia mara 35.

Uwezo wa Rice wa kukokota mpira uwanjani ulikuwa mkubwa zaidi msimu uliopita kuliko viungo wa Arsenal. kiungo huyo aliweza kukokota mipira mara 315, 65 zaidi ya Partey, 126 zaidi ya Odegaard, 232 zaidi ya Jorginho na 169 zaidi ya Xhaka.

Rice pia alikuwa na ufaulu bora zaidi wa pasi kwani alikamilisha asilimia 88 ya pasi zake aidha Partey aliweza kuimudu kwasababu alikuwa bora kuliko Odegaard (asilimia 84), Jorginho (asilimia 87.6) na Xhaka (asilimia 86.5).

Aidha Odegaard na Xhaka ndio waliofunga mabao mengi zaidi kwenye ligi kuliko Rice msimu uliopita huku wawili hao wakifunga jumla ya mabao 15.

GGML wameonesha njia udhibiti VVU - Dkt. Kikwete
Mikoa vinara ulimaji wa Bangi, Mirungi yawekwa hadharani