Klabu ya Manchester United ipo tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho wa kumnasa Declan Rice na kumfanya kuwa usajili wao mkuu kipindi cha majira ya joto ya kwanza chini ya kocha mpya Erik ten Hag, kwa mujibu wa 90Min.
90min anaelewa kuwa Rice na wawakilishi wake wameweka wazi kwa West Ham wanaona mwaka huu ni wakati mwafaka kwake kusonga mbele na kuendeleza kipaji chake sehemu nyingine.
West Ham walikuwa wameanzisha mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwaka jana, ingawa klabu hiyo inajua kwamba hawataweza kufikia mishahara anauotaka.
Inatarajiwa kwamba Rice ataweza kuweka mfukoni angalau pauni 250,000 kwa wiki tofauti na ule anaolipwa kule kwa wagonga nyungo.
David Moyes alipendekeza wiki iliyopita kwamba ingechukua pauni milioni 150 kumnunua Rice, lakini vyanzo vilivyo karibu vimethibitisha kwamba, mtu anayekaribia pauni milioni 120 atamwona mkuu wa Wagonga nyundo David Sullivan akiidhinisha uhamisho huo.
Pia ajirani wa Manchester City na wapinzani wa ligi Chelsea nao wanatajwa kuwania saini ya mchezaji huo.
Awali Liverpool walikuwa wameonesha nia ya kutaka kumnunua Rice mwaka jana, lakini gharama ya jumla ya mkataba huo inaonekana kuwaweka kando.