Kiungo mpya wa Arsenal, Declan Rice amesema kuna mengi zaidi kutoka kwake ambayo mashabiki hawayajui na kuwaomba wavute subira.
Nyuma ya paza inadaiwa kwamba Rice anaendelea kujifunza na kubadilika taratibu chini ya kocha Mikel Arteta.
Kiungo huyo aliyekiwasha West Ham United na kuisaidia kubeba ubingwa wa Conference League alisajiliwa Arsenal kwa rekodi ya usajili ya Pauni 105 milioni, lakini bado anaamini kiwango chake hakijaridhisha anavyotaka.
Lakini Rice, mwenye umri wa miaka 24 tayari amedhihirisha ubora kwamba anaweza kucheza nafasi tofauti atakayopewa na kocha.
Kutokana na mbinu ya ufundishaji ya Arteta, kiungo mwingine aliyesajiliwa kutoka Chelsea, Kai Havertz anasuasua na atabadilika taratibu.
Rice anaamini kiwango chake kitaimarika zaidi siku za usoni kufuatia kile alichoonyesha dhidi ya Crystal Palace mwanzoni mwa juma hii.
Nyota huyo amekiri kwamba mara nyingi wanafanya vikao na kutazana marudio ya mechi kama sehemu ya kujifunza ili kukabiliana na mikikimikiki ya mbio za ubingwa.
“Najisikia Vizuri sana. Nilikaribishwa kwa shangwe na mashabiki na wachezaji. Siwezi kuzungumza mengi kuhusu klabu hii kwa sababu nimejionea mwenyewe,” amesema