Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael A. Battle, amesema Demokrasia ya nchi inapaswa kuendana na mazingira yake mahususi badala ya kutegemea kufanana duniani.
Akizungumza katika Mkutano wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – TCD, Balozi Battle ametolea mfano kuwa Demokrasia ya Tanzania haiwezi kufanana na ile ya nchi za kifalme (kama Uingereza) na si lazima ifafane na mifumo mingine ya kiutawala inayotumiwa na nchi nyingine duniani.
Amesema, “Demokrasa ya Tanzania ni lazima izingatie muktadha na mazingira ya Tanzania, na iakisi matakwa ya watazania wenyewe. Nchi yotote duniani haina haki ya kuipangia Tanzania aina ya mfumo wake wa demokrasia.”
Aidha, Balozi Battle amesema Marekani inajivunia hatua kubwa alizochukua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha Demokrasia nchini Tanzania.