Deni la taifa la nje lilipungua kwa $619.4 (sawa na Sh 1.3 trilioni) katika mwezi Julai mwaka huu, ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imebainisha.
Kwa mujibu wa ripoti ya mapitio ya BoT, mabadiliko hayo yametokana pia na kushuka kwa thamani ya dola ya Marekani.
“Kupungua huko kumetokana kwa kiasi kikubwa na kushuka kwa thamani ya Dola dhidi ya fedha nyingine,” BoT imeeleza.
Imefafanua kuwa deni la taifa ambalo linajumuisha ukopaji wa sekta binafsi na sekta ya umma lilikuwa $19.8 bilioni mwezi Julai, ikishuka kutoka $20.5 bilioni ya Juni mwaka huu.
-
Jumaa Aweso awavuta wawekezaji katika sekta ya maji
-
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 4, 2018
Katika mkutano wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Juni mwaka huu, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa Serikali itatumia jumla ya Sh10 trilioni katika mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya kushughulikia madeni ya nje.