Kikosi cha mashetani wekundu, kimerejea nchini Uingereza kikitokea Marekani kilipokuwa kimeweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi, ambao unatarajiwa kuanza mwishoni mwa juma lijalo.

Kikosi cha Man Utd, kimerejea katika milki ya malkia Elizabeth, kwa kutua kwenye uwanja wa Manchester ambapo wachezaji wote walionekana ni wenye furaha huku mashabiki wakijitokeza kuwalaki.

Kubwa zaidi katika mapokezi hayo ambalo lilionekana kuwastaajabisha walio wengi ni vitu na mavazi ya gharama yaliyokuwa yamevaliwa na mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uholanzi, Memphis Depay.

Kwa tathmini ya haraka iliyofanywa na muandishi wa habari wa gazeti la Daily Mail, imebainika kwamba mshambuliaji huyo mpya wa klabu ya Man utd alikuwa amevalia mavazi pamoja na vitu vingine vyenye jumla ya thamani ya paund 9,923.

Sehemu ya mavazi ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, yaliyofanyiwa tathmini ni miwani yake ambayo imebainika inauzwa paund 388, saa ya mkononi inayouzwa 1999 pamoja na simu yake ya mkononi aina ya Golden Concept iPhone yenye gharama ya paund 4166.

Begi dogo la Depay alilokua amelibeba wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Manchester lina thamani paund 910 na kibegi kidogo cha kuwekea viatu kinauzwa paund 465 huku viatu vilivyokua vimevaliwa na mshambuliaji huyo vikiwa na thamani ya paund 1195.

Depay alijiunga na Man Utd mwezi Juni akitokea nchini kwao Uholanzi kwenye klabu ya PSV kwa ada ya uhamisho wa paund million 25.

Man ut watafungua msimu wa 2015-16 siku ya jumamosi kwa kucheza na Tottenham Hotspurs kwenye uwanja wa Old Trafford.

Liverpool Kumng’oa Young Old Trafford
Ndugai Adai Alipiga Simu Na Sio Mtu, Aliyeshambuliwa Atoa Ya Moyoni