Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) jijini Nairobi, nchini Kenya, imewakamata wahudumu wawili wa gari ya abiria ijulikanayo kama ‘matatu” waliomshambulia na kumpiga afisa mmoja wa polisi mjini Mombasa wakati afisa huyo akielekeza magari barabarani.
Kwa mujibu wa maafisa wa DCI, Emmanuel Lwamba na Nicholas Ngwava Peter, wanatuhumiwa kumpiga afisa wa trafiki katika kituo cha ukaguzi cha barabarani eneo la Mikindani Kaunti ya Mombasa wamekamatwa hatimaye.
Taarifa zinasema afisa huyo alikuwa akielekeza magari muda wa saa kumi na mbili na nusu asubuhi kwenye barabara ya Changamwe kuelekea Mikindani aliposhambuliwa na wawili hao.
Dereva na kondakta wake (makanga) wake wanasemekana kumvamia afisa huyo kwa ngumi na mateke kisha kutoroka na simu yake pamoja na shilingi elfu mbili alizokuwa nazo wakimwacha na majeraha puani na maumivu ya kifua.
“Msako wa wawili hao wanaohudumu kutumia gari la nambari ya usajili KBF 578K ulianzishwa na wao kushikwa saa chache baadaye,” DCI alisema.
Polisi wanaendelea kuwahoji wawili hao kubaini kilichosababisha wao kumshambulia afisa wa polisi.
Idara hiyo vilevile imetoa onyo kwa umma dhidi ya kushambulia maafisa wa usalama, ikisema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa kuwa ni hatia kubwa ambayo muhalifu na mkono mrefu wa sheria.
Ni nadra sana kukuta wananchi wanamshambulia askari wa polisi katika ameneo mengi au lah kunakua na sababu ambayo ilisababisha jazba kwa wananchi hao bila kujizuia.