Noel Cintron ambaye alikuwa dereva wa Rais wa Marekani Donlad Trump amemfungulia shitaka bosi wake kwa madai ya kutaka kuongezwa mshahara pamoja na malupulupu mengi yakiwemo kulipwa kwa kazi alizokuwa akizifanya katika muda wa ziada, na mengine hii ni kutokana na kumfanyia kazi kwa zaidi ya miaka 20 hadi alipoingia Ikulu mwaka 2016.
Katika shitaka lililofunguliwa na Noel amesema alikuwa akilipwa Dola $62,700 kwa mwaka na mnamo 2008 alilipwa Dola 68,000, na akapata nyongeza nyingine mwaka 2010 ambapo Trump hakumwongeza tena.
Ameongeza kwamba pamoja na mshahara huo kufikia Dola 75,000 kwa ongezeko la kawaida, alilazimishwa kulipia gharama za afya za kampuni la Trump Corporation ambazo zilifikia Dola 18,000 kwa mwaka.
Anadai pia amefanya kazi za ziada kwa muda wa saa 3,300 mnamo miaka sita iliyopita, na hivyo kwa mahesabu hayo anadai kulipwa kiasi cha Dola 178,000.
-
Video: Alichoongea Mwigulu baada ya kukabidhi ofisi kwa Lugola
-
Picha: Mwigulu Nchemba akikabidhi ofisi kwa Kangi Lugola jijini Dodoma
-
Video: Mtoto wa miaka 2 ajiua kwa risasi ya baba yake
Kufuatia madai hayo nimegundua kwamba Watanzania wengi bado hawafahamu haki zao kama wafanyakazi na ndio maana wafanyakazi wengi ambao wanafanya kazi katika makampuni binafsi mara baada ya kuacha kazi huendelea kuwa maskini kutokana na kwamba hawajui haki zao, angalu kidogo makampuni ya Serikali ambapo mtu mara baada ya kustaafu huwa na mfuko wa pensheni ambayo humsaidia kidogo kumsogeza maisha.
Watanzania ni maskini na kutokana na umaskini huo inapelekea muda mwingine tuone haya hata kudai haki zetu kwa waajili wetu kwa kuogopa kufukuzwa kazi.
Wapo watu katika makampuni mengi wanafanya kazi hata mpaka muda wao wa ziada bila kulipwa chochote, lakini wanaona ni sawa tu kutokana na kutokufahamu haki zao kama wafanyakazi, hasa hawa wafanyakazi ambao wapo katika ngazi za chini.
Lakini pia mfanyakazi ana haki ya kuongezwa mshahara katika kipindi cha muda fulani.