Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amefunguka kuhusu maisha ya kiungo Paul Pogba ambaye siku hadi siku amekua akitajwa kutofurahia maisha ndani ya Manchester United.

Deschamps amezungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakabali wa kiungo huyo, ambaye ni sehemu ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Ufaransa, kwa ajili ya michezo mitatu ya kimataifa dhidi ya Finland, Ureno na Sweden.

Kocha huyo amesema Pogba “hawezi kuwa na furaha” kwa hali yake ndani ya Manchester United. Wakati huu ambao Paul amehusika kwenye michezo 11 ya kikosi cha klabu hiyo ya England, akicheza michezo 5 pekee mpaka sasa.

“[Pogba] yupo kwenye hali ambayo hawezi kuwa na furaha ndani ya klabu yake, sio kwa muda anaopewa kucheza au nafasi anayopewa uwanjani.”

“Hayupo katika ubora wake. Alikuwa na majeruhi lakini pia aliugua COVID19 ambayo ilimsumbua sana, anahitaji muda kurudisha ubora wake.”

“Kwa upande wangu hakuna tatizo kama hilo. Mchezaji akiwa hana furaha kwenye klabu yake, atakuwa na furaha kuitumikia timu ya Taifa ya Ufaransa.

“Atanieleza anavyojisikia na kama ninavyomfahamu vizuri, itakuwa na matokeo chanya.” Amesema Deschamps.

Kikosi cha Ufaransa kilichoingia kambini kwa ajili ya michezo dhidi ya Finland, Ureno na Sweden.

Makipa: Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille), Mike Maignan (Lille) na Benoît Costil (Bordeaux).

Mabeki: Lucas Digne (Everton), Léo Dubois (Lyon), Lucas Hernandez (Bayern Munich), Presnel Kimpembe (PSG), Clément Lenglet (Barcelona), Benjamin Pavard (Bayern Munich), Raphaël Varane (Real Madrid) na Kurt Zouma (Chelsea).

Viungo: NGolo Kanté (Chelsea), Steven NZonzi (Rennes), Paul Pogba (Manchester United), Adrien Rabiot (Juventus), na Corentin Tolisso (Bayern Munich).

Washambuliaji: Wissam Ben Yedder (AS Monaco), Kingsley Coman (Bayern Munich), Nabil Fékir (Real Betis), Olivier Giroud (Chelsea), Antoine Griezmann (Barcelona), Anthony Martial (Manchester United), Kylian Mbappé (PSG) na Marcus Thuram (Gladbach).

Ansu Fati hadi Machi 2021
KMC FC kuivutia kasi Namungo FC