Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema hana budi kuangushiwa mzigo wa lawama, baada ya kikosi chake kutupwa nje ya Fainali za UEFA Euro 2020, usiku wa kuamkia leo.

Deschamps amesema anapaswa kubebeshwa mzigo wa lawama, kutokana na jukumu lote la timu ya taifa ya Ufaransa kuwa chini yake tangu alipotangaza kikosi kwa ajili ya fainali hizo.

Amesema Wachezjai wake walipambana kadri walivyoweza na yeye kama Kocha Mkuu alijitahidi kubuni mbinu mbadala za kuwashinda wapinzani, lakini mambo yaliwaendelea vigumu hadi dakika 120.

“Hilo siyo swali. Kuna Umoja na mshikamano kwenye hichi kikosi. Nina wajibika pale mambo yanapoenda vibaya. Niko pamoja na wao na wenyewe wako pamoja na mimi. Inaumiza, lakini tunahitaji mda zaidi kulirekebisha hili,” amesema Didier Deschamps

Ufaransa imeondolewa kwenye fainali hizo kwa changamoto ya mikwaju ya Penati 5-4 dhidi ya Uswiz, baada ya kwenda sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 120.

Baada ya kuiondoa Ufaransa kwa penati 5-4 , kikosi cha Uswiz kimetinga hatua ya Robo Fainali na kitacheza dhidi ya hispania.

Azam FC yaapa kulipa kisasi
Mbappe: Naomba mnisamehe