Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amesema hawezi kukubali kwamba Lionel Messi ndiye mchezaji bora zaidi kuliko Cristiano Ronaldo na Kylian Mbappe.

Hiyo imekuja baada ya Messi kutangazwa kuwa mshindi wa Ballon d’Or kwa mara ya nane, akiwa ndiye kinara, huku Ronaldo akifuatia kwa kubeba tuzo hiyo mara tano, Mbappe bado Hajafanikiwa kuibeba.

Mbappe ambaye alikuwa na kikosi cha Ufaransa kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2022, alishuhidia wakipoteza mchezo wa mchezo wa Fainali dhidi ya Argentina ya Messi.

Licha ya mafanikio ya Messi katika maisha yake ya soka, Deschamps amesema hadhani kama mshambuliaji huyo wa zamani wa Paris Saint-Germain anaweza kuchukuliwa kuwa bora zaidi wakati wote.

“Waargentina wanasema kwamba Messi ndiye bora zaidi wakati wote, lakini ni vigumu kusema kwamba Messi ni bora kuliko Cristiano Ronaldo au Kylian MbappĂ©, ambaye ni mdogo,” amesema Deschamps.

Katika tuzo za Ballon d’Or zilizotolewa mapema juma hili na Messi kushinda ya nane, MbappĂ© alishika nafasi ya tatu nyuma ya Erling Haaland wa Manchester City aliyemaliza wapili.

DC Twange aukataa urasimu kwenye Biashara, Uwekezaji
TFF, ZFF kuunda timu ya Taifa 'Taifa Stars'