Uongozi chama cha soka nchini Ujerumani (DFB) umeonyesha kuwa na imani na kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Joachim Low, licha ya tetesi kueleza kuwa huenda angesitishiwa mkataba wake.
Tetesi za kocha huyo alietwaa ubingwa wa dunia mwaka 2014 nchini Brazil, ziliibuka baada ya kikosi chake kufanya vibata kwenye michuano ya Ligi ya mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League).
Bodi ya uongozi wa DFB imesisitiza kumuamini kocha huyo na kuendelea kumpa ushirikiano, hatua ambayo imezima tetesi zilizokua zikimkabili kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari.
Ujerumani ilipoteza mchezo wa UEFA National League kwa kufungwa mabao sita kwa sifuri dhidi Hispania na kushindwa kusonge mbele kwenye michuano hiyo.
Kipigo hicho kilikua kikubwa kwa timu ya Ujerumani tangu wapoteze kwa Austria idadi kama hiyo ya magoli mchezo wa kirafiki mwaka 1931, lakini pia golikipa Manuer Neuer ameweka rekodi mpya kwa magolikiapa wa Ujerumani kwa kushinda mechi 96 na kuruhusu magoli sita katika mechi za ushindani kwa mara ya kwanza katika soka lake.
Kocha wa mabingwa wa soka nchini England Liverpool FC Jurgen Klopp juma lililopita aliulizwa kama kuna uwezekano wa kumabadili Low. “Kwa baadaye? labda ,” alijibu. Kwa sasa? Hapana.”