Baada ya kitendawili kudumu kwa muda mrefu, wengine wakisema huenda akatua Young Africans  na wenginge wakimhusisha na Simba SC, hatimaye, fumbo limefumbuliwa kwa mshambuliaji nyota wa Azam FC, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast ambapo rasmi ametua katika kikosi cha Al Nahdha FC ya Oman.

Baada ya ligi kuu Tanzania bara kumalizika Mwezi Mei mwaka huu, Kipre ambaye alibakiwa na mkataba wa mwaka mmoja na Azam FC alionesha nia ya kutoendelea na mabingwa hao wa Soka Afrika Mashariki na kati.

Kusisitiza kwamba alikuwa hataki kubakia Chamazi, Tchetche aliyekuwa mshambuliaji tishio kwa Mabeki hakurejea nchini kuendelea na maandalizi ya msimu mpya kama alivyofanya pacha wake, Michael Balou ambaye alishajiunga na kikosi cha Azam FC chini ya kocha Mhispania, Zeben Hernandez.

Awali Azam FC ilitangaza kwamba Tchetche hatakwenda popote kwasababu ana mkataba nao, lakini ametambulishwa jijini Muscat kujiunga na Al Nahda, moja ya klabu kubwa zinazochipukia nchini humo.

Jeshi La Polisi Lamshikilia Rais Wa Klabu Ya Simba
Wafugaji wakubwa watakiwa kujiandaa kwa ufugaji wa kisasa