Uongozi wa klabu ya Manchester United umeanza mazungumzo na FC Barcelona ili kufanikisha usajili wa mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Ousmane Dembele.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amekua na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Barca, hivyo Manchester United wameonea ni muda muafaka wa kujaribu kumsajili ili kuboresha kikosi chao.

Hata hivyo Manchester United wameanza mazungumzo hayo wakiwa na dhamira ya kumsajili Dembele kwa mkopo.

Katika hatua nyingine klabu ya Manchester United imezikana taarifa za kumsajili beki wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles.

Tangu jana taarifa zinaeleza kuwa Manchester United wapo mbioni kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 23.

John Legend na mkewe wapata Pigo
Safu ya ushambuliaji yaipa jeuri Azam FC