Wabunge wa Bunge la Tanzania, wameendelea na Vikao ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya awali kutoka nje kwa dakika kadhaa, kufuatia mlio wa sauti uliokuwa ukiashiria hali ya hatari kusikika bungeni.

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Akson aliwataka wabunge kutoka nje ya ukumbi na kukusanyika katika eneo la dharula na wakarudi kuendelea na vikao, baada vyombo vinavyohusika kuchunguza na kubaini hakukuwa na hatari.

Mpema hii leo Juni 27, 2023 Spika Dkt. Tulia Ackson aliahirisha kikao cha bunge kwa muda, kufuatia mlio wa kengele hiyo ya dharura, kuashiria hatari ambapo alielekeza kuwa Bunge litarejea tena baada ya dharura hiyo kutatuliwa.

Hali hiyo, ilizua taharuki kwa baadhi ya raia nchini ambao walikuwa na shauku ya kutaka kujua ni kipi kimesababisha hali hiyo, na majibu ya maswali yao yamepatikana na sasa kiu yao ni kuona wanaendelea kuwakilishwa vyema na Wabunge wao.

Aliyekufuru Dini apigwa mawe hadharani, afariki
Waziri Biteko: Madini kusababisha migogoro ya kisiasa