Angel Di Maria na Leandro Paredes Wanatarajiwa kuondoka ndani ya Klabu ya Juventus mwisho wa msimu.
Di Maria mkataba wake unamalizika kikosini hapo, hivyo atakuwa mchezaji huru.
Lakini Paredes alikuwa kwa mkopo ndani ya Juventus akitokea Klabu ya Paris Saint- Germain.
Wakati Di Maria akiwa huru, Paris Saint-Germain wametajwa kuwa wana mpango wa kumuuza Paredes baada ya kumaliza muda wake wa mkopo Juventus.
Imeelezwa kabla ya Paredes kuondoka, Juventus watapewa muda wa kufanya maamuzi kama wanamuhitaji moja kwa moja.
Hata hivyo, Di Maria ambaye yupo huru anatajwa kuwa tayari ameanza kuangaliwa na timu za Saudi Arabia ingawa yeye anataka kusalia Barani Ulaya.
Lakini kwa Paredes haijafahamika kama Paris Saint-Germain wamepata ofa yoyote mpaka sasa.