Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini, Abdul Naseeb maarufu kama Diamond Platinumz ameachiwa kwa dhamana kufuatia kesi inayomkabili ya kutumia mtandao wa kijamii kuweka picha akiwa faragha.
Diamond alikamatwa jana na jeshi la polisi kwa mahojiano kufuatia picha hizo zilizoonekana kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa ametoa taarifa hiyo na kusema kuwa wamemuachia kwa dhamana huku upelelezi ukiwa unaendelea, amesema kuwa ukikamilika msanii huyo atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Aidha Waziri wa Habari, Sanaa, Utamadani na Michezo, Harrison Mwakyembe wakati akijibu hoja ya Goodluck kuhusu matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii amesema kukamatwa kwa Diamond ni matokeo ya kanuni za maudhui ya mitandao ya kijamii zilizosainiwa hivi karibuni na kuwezesha sheria iliyotungwa tangu mwaka 2010 kuanza kufanya kazi.
-
Diamond akamatwa, ahojiwa kwa video za faragha
-
Video: Diamond Platnumz, Nandy watiwa mbaroni kwa kusambaza video chafu