Bosi wa WCB, Diamond Platinumz amefanya video na ‘Big Boss’ wa MMG, Rick Ross  nchini Marekani kukamilisha mradi wa ngoma yao mpya.

Mameneja wa Diamond Platinumz, Babu Tale na Sallam wamekuwa wa kwanza kuweka picha na vipande vya video ambavyo vinaonesha wawili hao wakishuti video hiyo, Miami.

Diamond Platnumz x Rick Ross On set now somewhere in Miami #BlackBottleBoys and we never stop!!

A post shared by “Mendez” 🔑 (@sallam_sk) on


“Diamond Platinumz na Rick Ross wakiwa kwenye eneo la tukio muda huu hapa Miami #BlackBottleBoys na hatutasimama kamwe!” Yanaeleza maandishi ya Sallam kwa tafsiri isiyo rasmi.

Msanii wa WCB, Ray Vanny ameonekana katika baadhi ya picha akiwa na Diamond na Rick Ross. Ray aliambatana na Baba Tiffah nchini Marekani kwenye tuzo za Afrimma.

Diamond ambaye alikuwa nchini Marekani mapema mwezi huu kwa ajili ya kushiriki tuzo za Afrimma, ametumia nafasi hiyo kumaliza kazi hiyo na Rick Ross ambaye ni balozi mwenzake wa kinywaji cha Luc Belaire.

‘Collabo’ hii kubwa kwa Diamond inakuwa miongoni mwa zile kubwa alizowahi kufanya na Wamarekani ikiifuatia ile aliyofanya na Neyo.

 

Juan Antonio Pizzi akubali lawama, kujiweka pembeni
Uchanguzi Kenya bado kitendawili