Mtoto wa Diamond, Tiffah Naseeb ambaye alianza kuwa staa akiwa na siku moja tu tangu azaliwe anaye ndugu yake wa damu ambaye licha ya kutokuwa staa, hafahamiki kabisa hata kwenye mtaa anaoishi kuwa ni mtoto wa Supa Staa. Diamond amebainisha.

Diamond alifichua siri hiyo hivi karibuni katika mahojiano na kipindi cha Papaso kinachorushwa na TBC FM.

Alisema kuwa alimpata mtoto huyo baada ya kujihusha kimapenzi usiku mmoja tu na mrembo mmoja alipoenda kufanya show jijini Mwanza mwaka 2010.

Alisema kuwa msichana huyo alimueleza kuwa ana mimba yake siku chache baadae na kwamba baada ya mabishano ya muda, alikubali kuanza kumhudumia kwa siri huku akisubiri mwanae.

Anasema baadae msichana huyo aligundua kuwa ameanzisha uhusiano na msichana mwingine na hayuko ‘serious’ na maisha ya mwanae. Kwa ushauri wa wazazi wake alianza kumuweka mwanae mbali na Diamond na hata kumdanganya kuwa hana mtoto kwa kuwa alitoa ujauzito.

“Siku moja nikaenda nikambanabana ‘nikamwambia wewe una mtoto’ akanikatalia kwasababu aliniambia ile mimba niliitoa nini, kumbe ni muongo. Nikaja nikamchunguza kumbe alikuwa amezaa na mtoto namuambia ‘nataka basi nimuone mwanangu’ alinikatalia sana lakini baadaye akaja kuniambia ni kweli ni mwanao umefanana naye na nini. Nikamwambia namuomba nimuone kwenye picha huku na huku hakuweza kuwa nayo,” Diamond aliiambia Papaso.

Harakati za kumuona mtoto wake ambaye hivi sasa ana umri wa miaka mitano hazikuwezekana hadi leo ambapo wengi walihisi ana mtoto mmoja tu ambaye ni Tiffah.

“Ikabidi asubuhi alipotoka hotelini akaenda kuniletea picha za mwanangu nione. Sasa wakati anakuja akaja amechelewa kwasababu mimi ndege yangu ilikuwa imeshakaribia ikabidi mimi nikarudi nikaacha vitu vyake pale reception, kurudi nampigia simu nitumie kwenye email sasa suala likaishia hivyo, yaani kila nikimpigia hapokei.” alisimulia.

 

 

 

Mtarajiwa Wa Kundi C Daraja La Kwanza Bado Kitendawili
Mhariri wa Gazeti la Mawio Azungumzia Kufutwa kwa gazeti lake