Hatimaye mvutano kati ya Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shoza umemalizika baada ya kufikia maridhiano kati ya mwimbaji huyo na wizara hiyo.

Mkutano huo uliofanyika jana ukiongozwa na Waziri mwenye dhamana, Dkt. Harrison Mwakyembe umemaliza mvutano wa maneno ulioibuka baada ya wizara kupitia Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuzifungia nyimbo kadhaa za wasanii ikiwa ni pamoja na nyimbo za Diamond, Wakawaka na Halleluyah.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao chao cha ndani, Waziri Mwakyembe alisema kuwa wamewekana sawa na msanii huyo na kwamba hivi sasa atakuwa akiiwakilisha nchi katika mstari mzuri zaidi kimaadili.

“Diamond ametuhakikishia mimi pamoja na naibu waziri kuwa tutashirikiana katika kusimamia maadili ya kazi za sanaa na yeye kuwa mfano mzuri katika kulinda utamaduni wa Tanzania,” alisema Dkt. Mwakyembe na kuongeza kuwa msanii huyo atakuwa balozi mzuri wa maadili.

Aidha, Dkt. Mwakyembe alisitiza kuwa Serikali haina mgogoro wowote na wasanii bali ina tatizo na mmomonyoko wa maadili katika sanaa.

Naye naibu waziri Shonza alisema kuwa Serikali na kundi la WCB kwa pamoja wameridhia hoja zilizotolewa na pande zote mbili na kwamba alichokisema Dkt. Mwakyembe ndio msimamo wa wizara.

Diamond kwa upande wake, alisema kuwa anashukuru kwa hatua iliyofikiwa na kwamba kinachofanyika sasa ni kuiendeleza sanaa ambayo inatoa ajira nyingi kwa vijana kwa namna mbalimnbali.

 

Alichokiongea [Dkt Mwakyembe] hakusema kwamba yeye alichoongea, amesema kuwa tumekaa mle ndani tumezungumza sasa namna ya kuweka sanaa yetu mbele, wao kama wizara na sisi kama wasanii kwa sababu lengo letu wote ni kuona sanaa yetu inafika mbali,” alisema Diamond.

Mvutano wa Diamond na Serikali uliibuka baada ya msanii huyo kupitia kipindi cha The Playlist cha Times Fm kukosoa vikali uamuzi wa Naibu waziri Shonza kufungia nyimbo zake.

 

Hatimaye: Nyimbo 15 zilizofungiwa zafunguliwa rasmi kwa masharti
China yathibitisha ziara ya Kim Jong Un, ajipanga kumuona Trump