Kwa mara ya kwanza Diamond Platinumz ameielezea sura ya mwanae Tiffah aliyempata na mrembo wa Uganda, Zari.

Akiongea na E Fm, Diamond ambaye amekuwa akiificha sura ya mwanae tangu azaliwe wiki kadhaa zilizopita, amesema kuwa kauli za wazazi wake baada ya kuiona sura ya mjukuu wao zinadhihirisha moja kwa moja kuwa mtoto huyo ni damu yake.

“Unajua mtoto kama si wako ni rahisi tu kujua. Na unajua mzazi anakuwa mtu wa kwanza kugundua kama mtoto si wako,” alisema. “Tena wazazi wetu wa Kiswahili wanakuaga sijui na machale gani akiona kama anasema ‘baba copy sio yako’.”

Diamond alidai kuwa sura ya mwanae huyo ni kama nakala ya sura yake.

“Yaani Latti ukimuona kabisa utasema ‘huyo ni Platnumz’.

Diamond amewapuuza wale waliokuwa wanadai kuwa mtoto huyo sio wa kwake na kumtaka apime vina saba (DNA).

Joh Makini Atoa Mtazamo Wake Katika Siasa Zinazoendelea
Rostam Aibuka Na Kumjibu Dk Slaa