Msanii maarufu  wa bongo fleva Nasib Abdul ‘Diamond platnumz’ ameitika wito wa Serikali iliyomtaka kuhudhuria kwenye tamasha la utamaduni, Afrika Mashariki ‘JAMAFEST’ linaloanza septemba 21 hadi septemba 28 mwaka huu.

Wito huo kwa diamond ulitolewa hivi karibuni na Waziri wa habari sanaa, Utamduni na michezo Dk Harrisoni Mwakyembe ambao umemtaka mwanamuziki huyo mahiri  kuhudhuria uzindizi wa tamasha hilo septemba 22 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Diamond kupitia ukurasa wake wa instagram amekubali wito huo atakapomaliza show yake ya Iringa atarejea kwaajili ya tamasha hilo.

‘Ndugu zangu wa Iringa poleni kwani hatutokuwa na after part ilitakiwa ifanyike siku ya jumapili jioni hivyo tutakuwa na show moja tu pale Samora Stadium ili kijana wenu kesho jumapili niwahi Dar kufanya balaa’ aliandika diamond

Msanii huyo ambae amekuwa na mashabiki wengi anatarajiwa kuhudhuria tamasah la JAMAFEST kwa mualiko aliopewa na waziri wa michezo ni baada ya kumaliza show yake ya Wasafi Festival iliyofanyika katika Mkoa wa iringa siku ya jana.

MC Pilipili atangaza nia ya kuwania ubunge, ataja chama
Tahadhari 4 za kujikinga na ugonjwa sugu UTI