Hivi karibuni mwanadada na mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Zarina Hassan alitangaza kuachana na msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz, tukio ambalo liliibua hisia kubwa sana kutokana na siku hiyo ambayo ilikuwa jumatano Februari, 14 maarufu kama siku ya wapendanao.
Habari hiyo ilibeba ”Headlines” katika vyombo mbali mbali vya habari na hata katika mitandao ya kijamii huku nyota huyo wa Bongofleva, Diamond akiendeleza ukimya kuhusu tukio hilo hali iliyovuta taswira za wengi kuwa nikutokana na maumivu ya kuachwa.
Kufuatia hayo, Diamond leo amevunja ukimya kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuweka wimbo wa msanii kutoka wasafi aliyesajiliwa hivii karibuni, Marombosso unaojulikana kama ‘Nimekuzoea’, akiwa ameuambatanisha na maneno yafuatayo.
” Hayo Mashairi changanya na Ua Jeusi ….dah @Mbosso naona kama ulinitabiria mdogo angu” ameandika Diamond.
Katika wimbo wa Marombosso mashairi yake yanasema hivi.
”hujaacha tobo uliloniachia ni bonge la tundu, sina nyendo mama kuninnuia ni rahisi, gundu nakunywa gongo kujisaidia ni rahisi ni aibu ualongo kitanda changu ndio choo, we ndo sababu, botomu bimba, na zolela naumia sana nimekuzoea, ndoto za ajabu kichwani unakuja wewe sura yako, mshasomewa, vitabu bado vinasema wewe, nikifa maiti yako yeeeeh”.
-
Penzi la Diamond na Zari latia nanga, Zari aanika madudu ya Diamond
-
Video: Papii Kocha ahuzunisha dunia na wimbo wake mpya ”Waambie”
Ujumbe huo umepata maoni takribani 2456 hadi sasa, na moja ya watu waliotoa maoni katika ujumbe huo ni Aunty Ezekiel ambaye amecheka sana na kuandika hivi.
”Saizi yako pata black frw hilo kwanza” akimaanisha nii haki ya Diamond kupata hilo ua jeusi.’
Mashabiki wengine wamemtolea povu, huku wengine wakihisi wawili hao hawajaachana bali ni ile njia ya kutafuta kiki inayotumiwa na wasanii wengi ambao wanataka kutoa nyimbo.
Hivi karibuni Diamond ameweka wazi kuwa zimebaki siku 29 kuachia albamu yake ya ‘A boy From Tandale’, hivyo inafikirika kuwa mahusiano hayo kuvunjika ni moja ya kiki kusogeza kazi hiyo ya albamu.